11 Feb 2025 / 78 views
Martinez kutua Arsenal

Arsenal wako tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho msimu wa kiangazi kwa dau la £100m (euro 120m) kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, mwenye umri wa miaka 27.

Mshambulizi wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21, anasalia kuwa nambari tisa katika orodha ya wachezaji ambao Arsenal ina uwezekano mkubwa wa kuwasajili msimu katika msimu huu wa kiangazi huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa na uwezekano mkubwa wa kumpiga bei katika uhamisho wake.

Arsenal pia ilifanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa AC Milan na Uhispania Alvaro Morata, 32, wiki iliyopita kabla ya kujiunga na Galatasaray kwa mkopo. 

Manchester City wako tayari kushindana na Real Madrid kwa ajili ya kumnunua beki wa kushoto wa AC Milan Mfaransa Theo Hernandez, 27, iwapo watamkosa beki wa Juventus na Italia Andrea Cambiaso.

Kipengele cha kutolewa katika mkataba wa mshambuliaji wa Bayern Munich na England Harry Kane, 31, kitapungua kutoka £67m hadi £54m katika mwaka ujao.

Mkufunzi wa Chelsea Enzo Maresca anapanga kumtumia kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos mwenye umri wa miaka 20 ambaye kwa sasa yuko Strasbourg kwa mkopo katika kikosi chake cha kwanza msimu ujao.

Arsenal itatafuta kumsajili mlinda mlango wa Uhispania Joan Garcia, 23, kutoka Espanyol msimu wa kiangazi.

Chelsea ilishindwa katika jaribio jaribilo lake la kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Tottenham Mfaransa Mathys Tel, 19, kutoka Bayern Munich siku ya makataa.